Usawiri wa Madhara ya Udhalilishaji wa Watoto katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Asali Chungu
DOI:
https://doi.org/10.63104/suj.v10.i2.131Keywords:
Fasihi ya Kiswahili, unyanyasaji wa watoto, athari za kimwili, kiakili na kijamiiAbstract
Kutokana na ukubwa na upana wa masuala ya unyanyasaji wa watoto, pamoja na haja ya kuyashughulikia, waandishi mbalimbali wa riwaya za Kiswahili wameandika kazi za kifasihi zinazosawiri masuala ya unyanyasaji wa watoto na madhara yake. Mfano wa riwaya hizo ni MMMEZA FUPA (Hilal, 2019), Mtoto wa Mama (Shafi, 2028), MUNGU HAKOPESHWI (Bahroon, 2017), Vuta N’kuvute (Shafi, 1999) na Kuli (Shafi, 1994). Madhumuni ya makala haya ni kuchunguza usawiri wa madhara ya unyanyasaji wa watoto katika fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka katika riwaya ya Asali Chungu. Mbinu zilizotumika kukusanya data za utafiti ni usomaji makini wa riwaya teule na utafiti wa maktabani. Data za awali zilipatikana kwa usomaji makini wa riwaya teule na data za upili zitatokanana utafiti wa maktabani. Ukusanyaji wa data ulitumia mkabala wa kimaelezo, ambapo data za utafiti zilipatikana kimaelezo na sio kitakwimu. Vilevile ilitumika Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi ilitumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yameonesha athari za kimwili, kiakili na kijamii wanazopata watoto wanaofanyiwa vitendo vya udhalilishaji. Athari hizi ni pamoja na kupata ujauzito, maumivu ya mwili, madhara ya kiakili ambapo waathirika wa udhalilishaji huweza kujihusisha na ulevi na kujiingiza katika ukahaba, kujiua, kukosa mwelekeo katika maisha na kuwa na tabia zisizoendana na maadili ya kijamii. Hatimaye, utafiti huu umetoa mapendekezo manne, kwa waandishi wa kazi za fasihi, watafiti, taasisi na asasi zinazohusika na mustakbali wa watoto pamoja na wazazi na walezi ili kuzuwia na kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa watoto.
Downloads
References
Baharoon, Z. A. (2017). MUNGU HAKOPESHWI. Mkuki na Nyota Publishers, Ltd. Dar es Salaam. Barnett, M.D., Marsden, A., Katherin, B., E., Maciel, I. V., & Marsden, A. D. (2017). Primal scene
phenomenon: Witnessing parental sexual activity and sexual orientation. In Sexuality & Culture. Springer Science & Busines Media, LLC (Limited Liability Company). https://doi.org.10.1007/s12119-017-9458-2. (Imesomwa tarehe 22/09/2025)
Bushara, MOE, Khan W. A. (2024). Influence of Parents’ Behaviour and Practice on their Family Health, Archives of Farmacy Practice, 15(1), 91-96. Umm Al-Qurra University, KSA. https://doi.org/10.51847/kELuWk7v3W (Imesomwa tarehe 16/10/2025).
David, A. (2018). Why Suspending or Expelling Students often Does more Harm than Good. Royal Melbourne Institute of Technology University, Melbourne.
Fuluge, Adria. (2021). Usawiri wa mchakato wa kujiua katika riwaya teule za Euphrase Kezilahabi: Ni mwangwi wa mtanziko wa kijamii? Tasnifu Shahada ya Uzamivu, Chuo Kikuu Cha Dodoma. (Haijachapishwa).
Hilal, A. (2019), MMEZA FUPA. Mkuki na Nyota Publishers Ltd. Dar es Salaam.
Kendall–Tackett, K.A., Williams, L.M., & Finkelhor, D. (1993). Impact of sexual abuse on children: A review and synthesis of recent empirical studies. Psychological Bulettin, 113(1), 164-180
https://doi.org/10.1037/0033-2909.113.1.164 (Imesomwa tarehe 23/09/2025). Kezilahabi, E. (1988). Rosa Mistika. Dar es Salaam University Press, Dar es Salaam.
Meiliana, S. (2019). Sociology of Literature. Pustaka Mandiri, Jakarta. Mohammed, S.A. (2002). Asali Chungu. Ujuzi Educational Publishers Ltd, Kampala.
Shafi, A. (2016). Kuli, Longhorn Publishers Ltd, Nairobi.
Shafi, A. (2018). Mtoto wa Mama. Longhorn Publishers (Tanzania) Ltd, Dar es Salaam Stoltz, J.A., Shannon, K., Kerr, T., Zhang, R., Montaner, J.S., & Wood, E. (2007). Association
between childhood maltreatment and sex work in cohort of drug-using youths. Social science and medicine (1982), 65(6), 1214-1221.
https://doi.org/10.1016/j.socsimed.2007.05.005 (Imesomwa tarehe 16/11/2025). Tremaine, L. (1978). Literary sociology and the african novel: the theories of sunday anozie and
Lucien Goldmann. Research in African Literatures, 9(1): 31–45. http://www.jstor.org/stable/3818471 (Imesomwa tarehe 01/01/2022).
Trickett, P. K., Noll, J. G., & Putman, F. W. (2011). The impact of sexual abuse on female development: lessons from a multigenerational, longitudinal research study. Development and psychology, 23(2), 453-476
Williams, S. (2016). The role of problem behavior s in the pathway from abuse to prostitution. Walden University, Minneapolis