Umuhimu wa Uwiano kati ya Malengo mahususi na Mazoezi ya Stadi ya Kuzungumza kwa Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Kigeni
Abstract
Uwiano wa malengo mahususi na mazoezi ya stadi ya kuzungumza ni muhimu katika ufundishaji wa lugha ya kigeni. Wataalamu mbalimbali wamejadili dhana ya uwiano katika kusaidia ufundishaji na ujifunzaji wa lugha za kigeni. Miongoni mwao ni Kurt (2020), ambae aliweza kuthibitisha kwamba uwiano humsaidia kila mwanafunzi kupata matarajio ya kile anachofundishwa. Katika kuliangazia suala hili, makala hii inalenga kufafanua umuhimu wa uwiano kati ya malengo mahususi na mazoezi ya stadi ya kuzungumza katika darasa la wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Mwandishi wa makala hii ameelezea umuhimu wa uwiano huu kwa sababu uzoefu unaonesha kuna baadhi ya walimu wanaofundisha lugha za kigeni wanashindwa kuoanisha malengo mahususi na mazoezi ya stadi ya kuzungumza wakati wa ufundishaji. Hivyo, makala hii itaonesha njia za kutambua ikiwa malengo mahususi yamefikiwa, jinsi ya kuoanisha malengo mahsusi na
mazoezi ya kuzungumza pamoja na umuhimu wa uwiano kati ya malengo mahususi na mazoezi ya stadi ya kuzungumza. Data za utafiti huu zimekusanywa kupitia mbinu za usaili wa nusu funge na uchambuzi wa nyaraka. Data zimechambuliwa kwa kuzingatia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yamethibitisha kuwa walimu wana uelewa juu ya uwiano kwa kiwango cha kuridhisha. Hivyo, imependekezwa kuwa kituo kinachohusika kiongeze juhudi za kuhakikisha kinazidi kutoa mafunzo kwa walimu wake kuhusu uwiano katika ufundishaji wa lugha hasa uwiano wa malengo mahususi na mazoezi kwa ujumla
Downloads
References
- Ali, L. H. (2015). Changamoto na mbinu za kiisimu katika ufundishaji wa stadi ya mazungumzo kwa wanafunzi wa elimu ya awali. (Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
- Anuradha, R. V., Roman, G. & Hemamalini, H.C. (2014). Methods of teaching English. Neelkamal Publication.
- BAKIZA. (2010). Kamusi la Kiswahili fasaha. Oxford University Press.
- Bandara, D. & Wijekularathna, D.K. (2017). Comparison of student performance under two teaching methods: Face to face and online. The International Journal of Educational Research, vol 12 (1), pg 69-79.
- Brandl, K. (2007). Communicative language teaching in action: Putting principles to work. Upper saddle river.
- Burk, J. J. (2016). Language learning for real-world context. (Master’s research) Utah state University
- Chen, L. (1997). Distance delivery systems in terms of pedagogical considerations: A revolution. Educational Technology, vol 37 (4), pg 34-37.
- Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. (2013). Zungumza Kiswahili: Hatua ya kwanza. Educational Books Publishers Ltd.
- Corder, S. (1987). Error analysis and interlanguages. Oxford University Press.
- Disha, M. (n/d). Evaluation in teaching and learning Process.
- Ephraim, E. (2016). Upimaji na tathmini. https://www.sribd.com/ documen t /3299 12066/ upimaji- tathmini-pdf
- Garbade, M. J. (2018). Four tricks to know if eLearning objectives are met.
- Hattie, J. (2011). Feedback in schools. In R. Sutton., M. J. Hornsey. & K. M. Douglas (Eds.), Feedback: The communication of praise, criticism and advice. Peter Lang Publishing.
- Hussain, S. (2017). Teaching speaking skills in communication classroom. International Journal of Media, Journalism and Mass Communication, vol 3, issue 3, pg 14-21.
- Julien, G. & Dookwah, R. (2020). Student’s transition from face to face learning to online learning at higher education: A case study in Trinidad and Tobago. Academic Journals, vol 15 (8), pg 487-494.
- Jyotsna, M. & Rao, S. N. (2009). Methods of teaching English. New Era Publication
- Kawasaki, J. (2021). What is task based learning? A guide to the popular teaching method. https://bridge.edu/tefl/blog/what-is-task-based-learning/#
- Klippel, F. (1984). Keep talking: communicative fluency activities for language teaching. Cambridge University Press.
- Kurt, S. (2020). How can we align learning objectives, instructional strategies and assessment?
- Makame, K. O. (2019). Mkabala wa kimawasiliano katika ufundishaji wa lugha ya pili: Mifano kutoka ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni Tanzania. African Journals Online, vol 82 No. 1 (2019).
- Mayor, M. (2016). SMART objectives for smart teachers. Pearson
- Miles, D., Mesinga, J. & Zuchowski. (2018). Harnessing opportunities to enhance the distance learning experience of MSW students: An Appreciative Inquiry Process. Social Work Education, 37
(6), pg 705-717. https://doi.org/10.1080/02615479.2018.1447557
- Pearson. (2016). Providing educational feedback. https://www.pearson. com/content/ dam/one-dotcom/one-dot-com/us/en/pearson-ed/downloads/Feedback.pdf
- Qureshi, J.A. (2019). Advancement in massive open online courses (MOOCs) to revolutionize disruptive technology in education: A case of Pakistan. Journal of Education and Educational Development, vol 6(2), pg 219-234.
- Rubanza, Y. I. (2010). Masuala ya msingi katika utayarishaji wa majaribio kwa wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Kioo cha Lugha, Juz 8.
- Sadler, D. R. (1989). Formative assessment and the design of instructional systems. Instructional Science, vol 18 (2), pg 119-144.
- Senthamarai, S. (2018). Interactive teaching strategies. Journal of Applied and Advaned Research, vol3.
- Shute, V. (2008). Focus on formative feedback. Review of Educational Research. Princeton, NJ: Educational Testing Services. https://wwwresearchgate.net /publication/ 220017728_Focus_on_ Formative_Feedback
- Sheeba. (2017). Importance of testing and evaluation in teaching and learning. International Journal of Society and Humanities, vol 11, No 1, pg 1-9.
- Timothy, K. M. (2016). Maana ya usemi na mazungumzo katika mitandao ya kijamii husuani Facebook na Twitter (Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu cha Nairobi.
- Wanjohi, J. M. (2014). Research objectives. http://sps.uonbi.ac.ke.